Machapisho yanayopendwa

6/recent/ticker-posts

MEDALI YA MTAKATIFU BENEDIKTO

Medali ya Mtakatifu Benedikto ni kisakramenti  chenye nguvu kubwa, hasa kwa wale wanaotafuta uponyaji wa magonjwa na kuondolewa katika vishawishi vya shetani.

Katika kueleza hili ni muhimu kukumbuka kwa kuwa medali huu ni moja ya kisakramenti, na visakramenti havitoi neema ya Roho Mtakatifu kama sakramenti; lakini kwa sala ya kanisa, vyatutayaharisha kupokea neema na vyatuwezesha kushirikiana nayo. Nguvu zake hazitokani na uzuri wake, au hata sala iliyoandikwa juu yake, bali nguvu za medali huo zinatokana na  sifa za Kristo Yesu, maombi yenye nguvu ya Mtakatifu Benedikto, baraka za Kanisa na imani na mwelekeo wa mtu anayeitumia medali hiyo. Medali huu hautumiki kwa ushirikina bali kwa imani, kama mwanamke mwenye kutokwa na damu aliyeamini kuwa uponyaji wake unaweza kupatikana kwa kugusa tu pindo la vazi la Kristo, au kama wale walioponywa na kuondolewa mapepo kupitia kitambaa kilichogusa mwili wa Mtakatifu Paulo (Rejea Matendo ya mitume 19:12).

Maana ya medali wa Mtakatifu Benedikto?

Medali hii ya Mtakatifu Benedikto imejaa alama nyingi. Kila sehemu inawakilisha kipengele fulani cha maisha ya Mtakatifu Benedikto au  maana maalumu ya kiroho.

Hapa kuna maelezo ya vipengele vya kawaida vinavyopatikana kwenye medali ya Mtakatifu Benedict:

Mbele ya medali:

1.        01. Picha ya Mtakatifu Benedikto; inawakilisha Mtakatifu Benedikto kama mwombezi mwenye nguvu dhidi ya uovu na chanzo cha mwongozo wa kiroho. Katika medali huu Mtakatifu Benedikto anaonekana akiwa  ameshikilia Kanuni iliyoandikwa ya Mtakatifu Benedikto katika mkono mmoja na msalaba mkono mwingine. Kwenye upande mmoja wa Mtakatifu Benedikto kuna kunguru. Upande mwingine kuna kikombe na nyoka akitoka ndani yake. Hii inawakilisha tukio katika maisha yake alipookoa maisha yake kimuujiza kutokana na sumu.

2.      02. Juu ya kikombe kuna maneno: "Crux sancti patris Benedicti," ambayo inamaanisha, "Msalaba wa Baba Yetu Mtakatifu Benedikto."

3.      03.Pembezoni mwa Mtakatifu Benedict kuna maneno, "Eius in obitu nostro praesentia muniamur!" ambayo inatafsiriwa kama, "Tuimarishwe  kwa uwepo wake wakati wa kifo chetu."

 

 Nyuma ya medali:

4.      04. Msalaba:  unaashiria ushindi wa Kristo dhidi ya dhambi na kifo kupitia kusulubiwa kwake.

5.   05. Wima wa msalaba una herufi "𝗖.𝗦.𝗦.𝗠.𝗟.," ambazo zinawakilisha "𝗖𝗿𝘂𝘅 𝗦𝗮𝗰𝗿𝗮 𝗦𝗶𝘁 𝗠𝗶𝗵𝗶 𝗟𝘂𝘅" ("Msalaba Mtakatifu uwe nuru yangu").

6.    06. Ulalo wa msalaba una herufi "𝗡.𝗗.𝗦.𝗠.𝗗.," ambazo zinawakilisha "𝗡𝗼𝗻 𝗗𝗿𝗮𝗰𝗼 𝗦𝗶𝘁 𝗠𝗶𝗵𝗶 𝗗𝘂𝘅", au, "Ewe joka  usiwe kiongozi wangu." Hii  inaoanesha ishara ya kukataa uovu.

7.       07. Herufi kubwa zinazozunguka msalaba wa katikati, "𝗖 𝗦 𝗣 𝗕", zinawakilisha: 𝗖𝗿𝘂𝘅 𝗦𝗮𝗻𝗰𝘁𝗶 𝗣𝗮𝘁𝗿𝗶𝘀 𝗕𝗲𝗻𝗲𝗱𝗶𝗰𝘁𝗶, ambayo inamaanisha, "Msalaba wa Baba Yetu Mtakatifu Benedikto."

8.   08.Juu ya medali kuna neno, "𝗣𝗔𝗫" ambalo linamaanisha "amani."

9.      09.Maneno yanayozunguka nyuma ya medali ni, "𝗩 𝗥 𝗦 𝗡 𝗦 𝗠 𝗩 - 𝗦 𝗠 𝗤 𝗟 𝗜 𝗩 𝗕". Hii inaashiria sala ya Kilatini ya ulinzi: "𝗩𝗮𝗱𝗲 𝗥𝗲𝘁𝗿𝗼 𝗦𝗮𝘁𝗮𝗻𝗮! 𝗡𝘂𝗻𝗾𝘂𝗮𝗺 𝗦𝘂𝗮𝗱𝗲 𝗠𝗶𝗵𝗶 𝗩𝗮𝗻𝗮!". Inatafsiriwa kama: "Ondoka, Shetani! Usinijaribu kamwe na uovu wako!".


Medali hii Inatumika kama kumbusho la kudumu la uwepo wa Mungu, ushindi wa Msalaba, na maombezi ya Mtakatifu Benedikto dhidi ya uovu.

Post a Comment

1 Comments