Machapisho yanayopendwa

6/recent/ticker-posts

ABOUT US


Karibu kwenye Blogu Yangu, NURU YA MARIA!

Naitwa JUSTINE BYABATO, mkatoliki na mwanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Napenda kuona jinsi imani yetu inavyoweza kuwa msukumo wa mabadiliko chanya katika maisha yetu ya kila siku. Kama Mkatoliki, upendo wangu kwa Mama Maria unaniongoza katika kuelezea kwa moyo jinsi tunavyoweza kushirikiana naye katika safari yetu ya kiroho. Imani yangu inanipa nguvu na mwongozo, na ninafurahi kugawana safari yangu na wewe.

Blogu yangu inachipua kutoka moyo wangu wa Mkristo na mapenzi yangu kwa Mama Bikira Maria. Ninapenda kuhamasisha wengine kushiriki ibada mbalimbali kwa Bikira Maria, sala, na kujifunza jinsi tunavyoweza kufuata mfano wake kwa upendo na unyenyekevu.

Karibu kushiriki nami katika NURU YA MARIA, ambayo ni sehemu ya kugundua mwanga wa imani yetu kupitia Mama Maria.

Asante kwa kuchagua kushiriki nami katika safari hii ya kiroho inayomwelekea Mama Bikira Maria, mlinzi wetu na msaada wa kila siku. Nuru ya Maria ni mahali pa kutafakari, kuelimishana, na kuguswa na uzuri wa ibada zinazomuhusu Mama wa Mkombozi.

Katika blogi hii  lengo langu kubwa ni kuhamasisha imani yetu kupitia Mama Maria kwa kufanya yafuatayo;

1.        Ibada Za Bikira Maria: ninaangazia ibada mbalimbali zinazomhusu Mama Bikira Maria na jinsi zinavyotuunganisha naye. Ninashirikisha sala mbalimbali za Bikira Maria, sala za Rozari, na matukio mengine yanayohusiana na ibada za Bikira Maria.

2     Matokeo ya Bikira Maria: Nuru ya Maria inaelezea matokeo yote ya Bikira Maria katika  sehemu mbalimbali alizowahi kutokea hapa duniani. Tunashirikishana ushuhuda wa watu walioathiriwa na ibada za Mama Maria na jinsi imani yao imeleta mabadiliko chanya.

3  Mafundisho ya Kiroho: Ninatoa mafundisho ya kiroho yanayohusiana na Bikira Maria, kutusaidia kuelewa jukumu lake katika historia yetu ya wokovu na njia zinazotuunganisha naye kiroho.

4    Safari yetu Kuelekea Mbinguni: Ninajadili njia za kiroho na maadili yanayotufaa katika safari yetu ya kuelekea mbinguni. Kupitia maandishi ya Blogi hii, ninajitahidi kuhamasisha na kuongoza kila mmoja wetu kwa utakatifu kupitia msaada wa Bikira Maria

Ninakualika kushiriki: Ningependa kusikia kutoka kwako! Jisikie huru kushiriki ushuhuda wako, au maswali yoyote unayoweza kuwa nayo. Ninatamani Nuru ya Maria iwe mahali pa kujisikia karibu na kujengana kiroho kwa msaada wa Mama Maria.

Asante kwa kuwa nami katika safari hii ya imani. Nipo hapa kukuza uelewa wetu wa Bikira Maria na kushirikiana katika upendo wa Kristo.

Kwa upendo wa Maria,

Justine Byabato. 

Post a Comment

2 Comments

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. Hakika naiona imani yangu ikizidi kuwaka kwa mapendo kwa HUYU MAMA MTAKATIFU WA MUNGU. Hata katika nyakati nisizoweza, pale ambapo nilikata tamaa kupindukia MAMA WA MUNGU Akaja kunifariji kwa kunipatia yale ambayo niliyaomba kwa MUNGU BABA NA BWANA YESU kupitia Jina la MAMA YETU BIKIRA MARIA. Hakika YEYE NI MAMA YETU pia Anatupenda kwa upendo ule wa ajabu kuweza kuelezea. Moyo wangu unajaa shukrani Kwake. Aksante sana kaka Justine kupitia haya machapisho unanifanya nijiskie amani na furaha zaidi ya Kumtangaza MAMA WA MUNGU hata pale napokutana na upinzani kutok kwa baadhi ya watu wasiotambua bado umuhimu mkubwa sana Aliopo Nao MAMA WA MUNGU. Naamini nitatumia pamoja na hizi makala zako kuwajulisha watu juu ya MAMA MARIA na namna Anavotupenda na kutuombea daima.
    " Pumziko la Milele uwape ee BWANA na mwanga wa Milele Iwaangazie wapumzike kwa amani. Amina.

    ReplyDelete