Mara nyingi tunajadili ni nani anaweza kuwa mwanamichezo bora, mwanamuziki bora, mwandishi bora, mwanamuziki bora; pia, ni lazima isemwe, kuna mama bora. Kwa mbali na pekee yake Bikira Maria alikuwa, ni, na daima atakuwa, mama bora wa wote.
Huku
tukisema hivyo, Akina wote duniani wanapaswa kutambua ukweli kwamba Maria ni mama
bora wa wote na kuyatafakari maneno, matendo, ishara, sura, nia, na maisha ya
Maria ili waweze kuwa mama bora zaidi na Zaidi.
Maria
ni Mama wa Mungu na ni Mama wa Kanisa, lakini pia Maria ni Mama yetu mpendwa!
Tujaribu kumpendeza Maria, Mama yetu na hakika akina mama
wengi ulimwenguni watapiga hatua kubwa katika kuwa mama bora siku zote za
maisha yao!
Leo nitaelezea kwa namna ya pekee
njia kumi tofauti ambazo tunaweza kuonyesha upendo mkubwa kwa Mama Maria, na
kupitia maombezi yake yenye nguvu zaidi, atapata kwa ajili yetu neema bora
zaidi kutusaidia kuwa watakatifu ambao tunaitwa kuwa, na wengi wetu kama akina
mama.
1.
Zungumza Naye.
Tunapaswa
kuwa na desturi ya kuzungumza na Maria, Mama yetu mpendwa, mara kwa mara.
Kumweleza, kusema naye kwa moyo wetu, kumpenda, na kuweka maisha yetu yote
mikononi mwake ni jambo linalompendeza sana, pamoja na Mwana wake Yesu, Mwana
wa Mungu na Mwana wa Bikira Maria. Maria ni kielelezo chetu, mwongozo wetu,
rafiki yetu, na Mama yetu mpendwa. Anatupenda sana na anatamani kuwa na
mazungumzo mara kwa mara na sisi.
Tuanze
leo! Marafiki wazuri wanawaza kuhusu wenzao na kuzungumza mara kwa mara! Maria
ni Mama yetu, lakini pia ni rafiki na mshauri wetu.
2.
Anza Siku Yako na Maria
Kila
asubuhi tunapoamka, hatua yetu ya kwanza inapaswa kuwa sala, na ni sala gani?
Kwa nini usianze siku yako kwa kujitoa kabisa kwa Yesu, katika yote unayosema,
unayofanya na unayofikiria, kupitia Moyo Mtakatifu wa Maria? Mpe Yesu kupitia
Maria macho yako, masikio yako, akili yako, moyo wako, mwili wako, na hata nia
zako—kwa neno moja, mpe kila kitu kwa Yesu kupitia Mama Maria. Ni muhimu sana
kuanza siku yetu vizuri kupitia Moyo wa Maria!
Hapa
kuna sala ya Kujiweka
Wakfu kwa Maria. Ikiwa utapenda, unaweza kusali sala hii hapa chini. Ikiwa huna
skapulari
ya rangi ya kahawia, itapendeza
kununua moja na
kuvaa skapulari
ya Mama Maria kama ishara kwamba wewe ni wake na unakuwa chini ya ulinzi wake!
Vaa skapulari
wakati wote, isipokuwa wakati
wa kuoga.
Maria, Malkia wangu na Mama yangu, najitolea kwako kabisa. Kuonyesha ibada yangu kwako, nakutolea leo macho yangu, masikio yangu, kinywa changu, mwili wangu wote bila kizuizi. Kama vile mimi ni wako, Mama mpendwa, nihifadhi na unilinde kama mali yako na milki yako. Amina.
3.
Mwambie Mama Maria kuwa
Unampenda
Mama
kamwe hachoki kusikia mtoto akisema: "Mama, nakupenda sana; wewe ni
bora!" wakati mwingine
tunaweza kukumbana na kishawishi kwa kusema hivi: "Tayari anajua, kwa
nini kumwambia kitu ambacho tayari anakijua?" Kweli, mama mzuri labda
tayari anajua. Hata hivyo, bado anapenda kusikia maneno hayo. Kwa kusema: "Mama,
nakupenda sana", moyo wa mama yako utaruka kwa furaha.
Hivyo
ndivyo inavyopaswa kuwa kwa Mama yetu Mtakatifu. Kwa maneno rahisi kabisa
tunaposema: "Mama Maria, nakupenda", basi Maria, Mama wa
Mungu, hupata furaha kubwa katika Moyo wake safi na Mtakatifu. Hivyo, kila wakati, tukumbuke kusema: "Mama
Maria, nakupenda!"
4.
Tembea Naye
Kila tunaposafiri, iwe ni safari fupi au ndefu,
tunapaswa kumwalika Mama Maria atembee
Pamoja nasi. Yeye ni rafiki mwema katika safari na anaweza kutulinda kutokana na hatari
nyingi katika safari zetu, iwe ni hatari za kimwili au za kimaadili.
5.
Fuata Mfano wa Maria
Katika maisha yetu kuna wale watu Fulani tunawapenda
sana na kuwaheshimu sana , mara nyingi inatupelekea kuiga tabia zao na kutaka kufanana nao,
na tunapowaiga inapelekea kuitwa wafuasi wao. Mtakatifu
Louis de Montfort anasisitiza juu ya sifa kumi kuu za Maria ambazo tunapaswa
kujitahidi kuziiga: unyenyekevu wake wa dhati, imani hai, utii ulio kipofu, Roho ya kusali daima,
kujinyima, usafi ulio zaidi, upendo mkubwa,
uvumilivu wa kishujaa, wema wa kimalaika, na hekima ya kimbingu. (True devotion to Mary,
Mtakatifu Louis de Montfort #108)
6.
Kumtegemea na Kumkabidhi Maria
Ikiwa
tunamwamini mtu kwa dhati, basi tunaweza kumkabidhi mahangaiko yetu kwake,
tukiwa na hakika kwamba mtu huyu maalumu atatujali na kutulinda.
Fikiria hili, Mungu Baba alimkabidhi Mwana wake pekee katika ulinzi wa Maria.
Kwa hiyo, tunaweza kukabidhi
Maisha yetu katika ulinzi wa Maria, Mama yetu mpendwa na mwenye upendo
zaidi. "Haijasikika kamwe kwamba
ulimuacha mtu aliyekimbilia msaada na maombezi yako."
(Memorare, Mtakatifu Bernardo)"
7.
Mwambie Maria matatizo na maanguko yako
Tunaweza
kushawishiwa na adui, shetani, ambaye hakika anamchukia Maria, kujisikia
kizuizi katika kumwambia Mama Maria matatizo yetu na mateso makubwa. Badala
yake, iwe kinyume chake! Mama bora, Maria anajua vizuri kwamba wakati mtoto
anapoumia, na kujeruhiwa, ndipo anapohitaji upendo mwororo na msaada zaidi. Hivyo ndivyo
inavyopaswa kuwa kwetu!
Katika siku zinazoonekana kuwa na mawingu mazito, na kusikitisha kabisa
katika undani wa roho zetu, ndipo tunapohitaji kufungua na kuzungumza na Mama
Maria. Maria ni kimbilio kwa wenye dhambi na afya ya wagonjwa—hivi ni vyeo viwili kwa Maria katika
Litania zake maarufu!
8.
Mwite Maria Unapokuwa
majaribuni.
Maisha
yetu ni ya
mapambano ya mara kwa mara; sisi ni askari wa Yesu na Mama Maria pia. Hii
inamaanisha tuko kwenye uwanja wa vita wa mara kwa mara. Maadui wetu ni watatu:
shetani, mwili, na dunia. Tukijua ukweli huu wa kina wa vita vya kiroho,
tunapaswa kuliita
Jina Takatifu la Maria katika hali ya vita na ushindi utakuwa wetu!
Vita
vya Lepanto vilithibitisha ushindi mkubwa kupitia kumwita Maria na kusali Sala ya Rozari Takatifu, kwa
ushawishi wa Papa Mtakatifu Pius V. Tuweke matatizo yetu mikononi mwa Maria,
ambaye ni hodari kuliko jeshi lote lililo tayari kwa vita! Jina la Maria pekee
linaleta hofu na woga katika jehanamu yote
9.
Eneza Upendo kwa Maria Kama Mama
Ikiwa
kweli tumepata upendo wa Maria katika maisha yetu ya kila siku, bila
shaka tutataka kumfanya Mama Maria ajulikane kote. Maria hapendwi na kuheshimiwa kwa sababu moja kuu:
hajulikani! Anawezaje kujulikana? Kwa njia nyingi! Frisha kusoma vitabu vizuri
kuhusu Maria kama vile The Glories of Mary kilichoandikwa na Mt.
Alphonsus Liguori, True Devotion to Mary kilichoandikwa na Mt.
Louis de Montfort, na Mater Redemptoris na The Blessed Virgin Mary and the
Rosary vyote vilivyoandikwa na Papa Mtakatifu John Paul II.
Hamasisha
wengine kusali Sala Takatifu ya Rozari na kuisali kila siku,
toa Rozari pamoja na vipeperushi juu ya jinsi ya kusali Rozari, na mwishowe,
himiza kuvaa Skapulari
ya Rangi ya Kahawia ya Mtakatifu Wa Karmeli.
10.
Kufa Kwenye Mikono ya Maria
Wakati
muhimu zaidi katika maisha yetu ni wakati tunapokufa. Wakati huo utaamua kwa
milele, hatima yetu ya milele—au mbinguni au jehanamu. Kwa nini usijiandae kufa
kwa neema, kufa kifo kitakatifu, angalau mara 50 kwa siku? Jinsi gani, unaweza
kuuliza? Kwa kusali Rozari Takatifu kila siku. Kila wakati tunaposali Salamu
Maria, tunajiandaa kwa kifo kitakatifu na furaha na maneno haya: Maria Mtakatifu Mtakatifu Mama wa Mungu utuombee, sisi
wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. AMINA.
Kwa
hiyo, tufurahi kwa kutambua kwa kina kwamba sote tuna Mama wa mbinguni, Maria
Mama wa Mungu, Mama wa Kanisa, na Mama yetu mpendwa. Anatujua, anatujali,
anatulinda, lakini hasa, anatupenda! Kwa kweli, katika nyakati za majaribu,
mapambano, na vita vikali vya maisha, tutafute kimbilio letu katika Moyo
Mtakatifu wa Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu!
2 Comments
Thanks very much,let us live with Mother mary🙏🏼🙏🏼
ReplyDeleteThank you so much dear brother. Through these sweet messages by THE VIRGIN MARY'S Grace and prayers I am devoted to turning to JESUS CHRIST and THE HOLY BLESSED VIRGIN MARY I was at the very edge of being drowned deep into hell due to the worst life I have been leaving recently. But amazingly THE MOTHER OF GOD through Her Servant Dr. Justine D. Byabato I wonder why i feel touched by our HOLY MOTHER'S voice through Her servant. By Her Grace , I'll let the world know about Her and Her HOLY BLESSED SON JESUS CHRIST. THANK YOU SO MUCH BROTHER AND MAY SHE FILL YOUR WORLDLY DAYS WITH HER AMAZING LOVE AND GRACE so you may help the lost like me and others to follow the path to CALVARY where our True Faith , Love and Salvation belongs. Amen.
Delete