Machapisho yanayopendwa

6/recent/ticker-posts

SIKUKUU YA HURUMA YA MUNGU.

 



Huruma ya Mungu


Hii ni moja kati ya mambo makubwa sana katika ibada kwa Huruma ya Mungu iliyofunuliwa kwa Mt. Faustina. Kuanza kwa sikukuu hii kuliombwa na Bwana wetu Yesu Kristu kwa mara ya kwaza huko Plock, Polandi mwaka 1931, alipokuwa akiagiza picha ya Yesu mwenye huruma ichorwe Ninatamani kuwepo na Sikukuu ya Huruma. Ninataka picha hii utakayoichora, ibarikiwe katika jumapili ya kwanza ya Pasaka, jumapili hiyo ndiyo itakuwa jumapili ya Huruma ya Mungu.” (Shajara, 49).

Kuchaguliwa kwa jumapili ya kwanza ya pasaka kuwa jumapili ya Huruma ya Mungu kuna umuhimu wake kiteolojia, inaonesha uhusiano wa Karibu kati ya fumbo la pasaka na fumbo la Huruma ya Mungu. Uhusiano huu unaoneshwa kwa novena ya huruma ya Mungu inayoanza katika siku ya ijumaa kuu kama maandalizi ya sherehe hii.

Sikukuu hii ya huruma ya Mungu sio tu siku ya kumwabudu Mungu katika fumbo lake la Huruma bali ni muda wa neema kwa watu wote. Bwana Yesu alisema “ninataka  sikukuu ya huruma iwe kimbilio na makazi ya Roho zote, hasa za maskini wadhambi” (Shajara, 699). “Roho zinaangamia licha ya mateso yangu makali. Ninawapa tumaini la mwisho la wokovu, ambalo ni kuiomba huruma yangu. Kama hawatoiabudu huruma yangu, wataangamia milele”. (Shajara, 965, 998).

Ukubwa wa sikukuu hii unapimwa kwa  kipimo cha neema zisizo kawaida ambazo bwana ameziahidi; Yesu alisema “… Yeyote atakaye sogelea kisima cha uhai katika siku hii ataondolewa dhambi zake zote na adhabu zake zote” (Shajara, 300). “Katika siku hii kina cha huruma cha huruma yangu ufunguliwa. Ninamwaga Bahari ya neema kwa Roho zitakazo karibia kisima cha huruma yangu…” (shajara, 699).

Hivyo wapokeao komunyo takatifu katika siku hiyo hujaliwa neema ya pekee, neema ya ondoleo kamili la dhambi na adhabu zake. Neema hii ni kubwa zaidi kuliko rehema kamili, ambazo huondoa tu adhabu za muda za dhambi zilizotendwa, lakini hazitoi msamaha wa kosa. Hakika neema hii maalumu kabisa, inazidi hata rehema zile zitolewazo na sakramenti sita isipokuwa sakramenti ya ubatizo kwa sababu neema ya kuondoa dhambi na hatia ni tunda sakramenti ya ubatizo. Katika ahadi zilizotajwa hapo juu alisema komunyo takatifu katika sikukuu ya huruma itaambatana na neema hizo.

Ni wazi kwamba ili komunyo takatifu itoe ondoleo la dhambi na msamaha wa dhambi, lazima ipokelewe katika hali inayostahili ya hali ya neema ya utakaso Rohoni na katika kutimiza masharti muhimu ya Ibada ya Huruma ya Mungu. Ikipokewa isivyostahili katika hali ya dhambi bila tumaini katika huruma ya Mungu na bila tendo lolote la huruma kwa Jirani, badala ya kuleta neema za pekee sana inaweza kuleta hasira na ghadhabu ya Mungu kwa aliyekomunika (Maelezo ya Mwanateolojia wa Huruma ya Mungu, Padre  Ignacy Rozycki).

Katika Maisha ya leo tunaona dunia  inazama katika dhambi na mambo mengi sana maovu yanatokea, tunashuhudia damu wa Watoto wasiozaliwa (mimba zinazotolewa), wengi wanadhulumiwa na idadi  inaongezeka ya wakristo wanaojihusisha na kanisa juu juu tu au kutojihusisha kabisa. Wengi wanakaa miaka mingi bila kupokea sakramenti, hawashiriki Misa takatifu jumapili, hawabatizi Watoto wao, wala kujishughulisha na malezi ya Watoto kikristo. Mara nyingi tabia hii haitokani na nia mbaya bali uelewa mdogo au kutokuelewa kabisa umuhimu wa neema za huruma ya Mungu. Neema hizi hupatikana kwa wingi sana katika sakramenti zote na katika matendo mengine ya kiroho. Kutambua  ukuu wa huruma ya Mungu ndiko kunapaswa kulipia hasara inayoletwa na ubaridi na kutokujali kwa wakristo wa nyakati hizi.

Maandalizi ya sikukuu hii ni Pamoja na kufanya novena ya huruma ya Mungu kuanzia Ijumaa kuu hadi jumamosi kabla ya sherehe ya Huruma ya Mungu.

 

Post a Comment

0 Comments