Machapisho yanayopendwa

6/recent/ticker-posts

MOTO WA TOHARANI

 


Kanisa  linafundisha kuwa Roho  hutoka   Toharani punde tu  zinapokamilisha kusafishwa kwa moto. Toharani sio moto wa milele, ambapo Roho haiwezi kutoka. Ukiwa umezungukwa na moto unaofika ndani ya Roho yako, maumivu gani  unayoyapata! Moto wa kawaida unaunguza miili tu, Fikiria kwa jinsi gani moto wa toharani unavyokuwa nani anaweza kushika kaa la moto mkononi kwa dakika moja? Lakini moto wa toharani unashika Roho; unafika katika akili kumbukumbu na fahamu. Nani awezaye kustahimili moto huo?. Inasafisha Roho bila hata kuhiaribu.

Moto wetu si chochote ukilinganisha na ule wa toharani. Moto wa ulimwengu huu ni zawadi kutoka kwa Mungu, Moto wa  Toharani  uliumbwa kwa haki yake, moto wa toharani ni sawa na ule wa moto wa milele, isipokuwa mda wa kukaa huko ndio utofautiana, maumivu ya dunia hii  hayawezi kulinganishwa na yale ya   toharani.

Nani atakataa kusikia maombolezo yao? Fikiria kuwa kama  ungekuwa huko na hakuna mtu anayeonesha upendo kwako, unawezaje kuuona  ukatili huo? Fikiria vizuri kuhusu ili na   chukua hatua.

 

Mfano:

Stanislasi Kostka, Mjesuit kutoka Polandi, aliona Roho ya  toharani ikiwa imefunikwa kwa miale ya moto na ilikuwa ikipiga mayowe. Stanislasi aliuliza Roho hiyo kuwa moto huo ni kama wa duniani?.  Roho ilijibu kuwa moto wa duniani unapoulinganisha na moto wa Toharani, moto wa duniani ni kama jiwe laini la thamani. Haikuwa rahisi padri kuamini, padri Stanislaus alimwambia kuwa alikuwa anatoka kuonja kidogo moto huo, kama inawezekana.

“Ah! Mwanadamu aliyebado duniani hawezi kuhisi hata chembe ya moto huo. Lakini kama unataka kujua, nipe mkono wako nami nikuoneshe” ile roho ilisema.

Stanislas alipanua mikono yake ile Roho ilimwangushia tu tone la jasho lake wala haikumshika. Alipata maumivu makubwa Stanislas alipiga kelele kiasi kwamba alikuwa anataka kufa kwa haraka marafiki zake walikuja na aliwaeleza kilichotokea.

Wote waliogopa na kuchukua maamuzi ya kuongeza toba, kuachana kabisa na anasa za dunia hii, pamoja waliamua kumwambia kila mtu kuhusu moto wa toharani, ili watu waweze kujifunza jinsi ya kuepuka toharani. Mtakatifu    Stanislas aliishi mwaka mmoja zaidi akiwa na maumivu makali ya jeraha alilopata ambalo alikuweza kupona.

Padri Ferdinand wa Castile alilipoti ukweli  mwingine wa tukio lililotokea katika nyumba ya watawa., huko nchini uhispania.

Katika Konventi hiyo kulikuwa na mapadri wawili waliokuwa marafiki, na walipenda sana kuongea kuhusu mambo   mbalimbali. Waliahidiana kukumbukana iwapo wakifa.

Mmoja wao alifariki, na dakika chache baada ya kifo chake padri huyo  alimtokea rafiki yake baada ya kumsalimu, alimwambia rafiki yake kuwa anateseka sana kwa mda mrefu kwa sababu ya kosa dogo sana ambalo hakulilipia akiwa hai ili kumfanya rafiki yake amsaidie, alimwonesha miale ya moto, ambayo  ilikuwa ikimtesa alisema “Hakuna kitu  chochote duniani kinachoweza kukuelezea vizuri kuhusu moto huu. Je unataka nikuoneshe?” Roho hiyo  iliweka mkono wake katika meza cha kushangaza mkono huo ulitoboa meza na   kuzama chini.

Meza hiyo ambayo ni ushahidi wa moto wa toharani   imetunzwa huko Zamora uhispania.

Mungu anaweka Roho katika moto hadi inaposafishwa kabisa. Roho inapomalizia kusafishwa roho hiyo hukaa mbele ya Mungu na inaunganika na Mungu Roho hapo haiwezi tena   kuteseka bali inahisi moto wa mapendo ya Mungu.

Post a Comment

0 Comments