Bila 'fiat' ya
Maria (neno la Kilatini linalomaanisha idhini), tusingekuwa tunasherehekea
Krismasi au historia ya wokovu ingekuwa imeandikwa upya. Ndiyo jinsi jukumu
muhimu la Mama Maria lilivyokuwa.
Kujua mapenzi ya
Mungu si rahisi kama ilivyokuwa kwa kupashwa kwake Maria kuliko kuwa na msisimko. Alipokubali
mapenzi ya Mungu, alipitia vikwazo na majaribu mbalimbali, ingawa alikuwa mama
wa Masihi. Kwa mfano, alipojifungua Yesu, hakukuwa na nafasi inayopatikana
katika nyumba ya wageni. Aliridhika kumzaa mwana wake ndani ya hori ambapo
wanyama walikuwa wanajikinga. Kisha, Yesu alipokuwa na miaka miwili, Mfalme
Herode kwa wivu alitaka kumwondoa. Yusufu na Maria walilazimika kukimbilia
Misri ili kuepuka dhuluma za Mfalme Herode muuaji.
Nasi tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwa Maria tunaposherehekea kuzaliwa kwake, usisingizie wala
kukasirika wakati mambo hayaendi kama unavyotaka, mfano wakati ndoa inaporomoka, kupoteza kazi,
kushindwa kufaulu mtihani pale unapokuwa
na matatizo ya kifedha.Lakini usikubali tu hali yako, bali fanya kitu cha
kuiokoa. Yesu aliwahurumia wale waliokuwa wagonjwa kwa homa, kudondoka, upofu,
viwete, na aliwaponya. Tunapokutana na dhiki kubwa, tufikirie kumwendea Bwana.
Maisha
yanapokwenda vizuri, kumbuka kumshukuru Bwana. Hata hivyo, unapokutana na
changamoto, kumbuka kwamba Yesu, Maria, na Yusufu walipitia hali mbaya zaidi.
0 Comments