Imani yetu katoliki inafundisha kuwa Toharani ni sehemu ya mateso,
ambapo haki ya Mungu ulipwa.Ni toharani sio mbinguni ambapo kitu chenye uchafu
kinaweza kuingia, sio motoni ambapo
hakuna wokovu tena. Toharani ni sehemu ya katikati iliyopo kati ya furaha ya milele na mateso yasiyo na mwisho. Toharani hufanana moto wa milele kwa mateso
yake; hufanana mbingu kwa sababu ya
utakatifu wa Roho zilizoko huko.
Toharani ni moto
unaounguza lakini unasafisha, ni sehemu ya machozi, wakati usafishwaji
unapokamilika, Mungu anawaita karibu yake Roho zilizookolewa kwa mateso anaziunganisha pamoja na furaha yake.
Toharani ni
adhabu ya mda na haitakuwepo baada ya hukumu ya mwisho. Hii ndiyo toharani ni sehemu
ambapo baadhi ya Roho za watu waliokufa bado zinateseka kwa sababu kwenda moja kwa moja mbinguni ni
bahati iliyopo kwa watu wachache sana.
Baadhi ya
marafiki zetu wanaweza bado kuwa wako huko. Huko ndipo siku moja tutakwenda
itakuwa hivi punde tu. Ni muhimu sana kusali kwa ajili ya Roho ili kwamba
nasi tutakapokuwa huko waweze kutuombea.
Huko, Roho
zinaosha dhambi zao zote. Toharani inahitajika ili kukamilisha
toba, ambayo hatukuimalizia wakati bado tupo hapa duniani.
0 Comments