Machapisho yanayopendwa

6/recent/ticker-posts

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA PILI.

 


Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee mapadri wote na watawa. Uwazamishe katika kilindi cha huruma yangu isiyo na mwisho. Ni wao hasa walionipa nguvu ya kuweza kuyavumilia mateso yangu makali mno. Kwa njia yao, kama vile mifereji, huruma yangu humiminika na kuwatiririkia wote.”

Tuwaombee mapdri na  watawa wote wanawake ili wadumu kiaminifu katika utumishi wao na wakfu wa maisha yao kwa Yesu Kristu Bwana harusi wao.

Ee Yesu mwenye huruma tele, kwako hutoka mema yote. Uwazidishie neema yako watawa wanawake waliojitolea na kuwekwa wakfu katika utumishi wako, ili watekeleze utumishi wao kwa huruma na kwa jinsi inayofaa, na kwamba wale wanaowaona na kuzishuhudia kazi zao bora, waweze kumtukuza Baba wa Huruma aliye mbinguni. Amina.

Baba yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …

Baba wa Milele, elekeza macho yako yenye huruma, juu ya jeshi teule la wafanyakazi shambani mwako. Uzitazame kwa wema roho zao mapadre na watawa wote. Uwajalie wingi wa Baraka zako. Kwa njia ya upendo wa Moyo wa Mwanao, humo ambamo wameingizwa, uwape nguvu na mwanga, ili waweze kuwaongoza wengine katika njia ya wokovu, na kwa sauti moja, waihimidi huruma yako kwa nyimbo za sifa bila mwisho. Amina.

Post a Comment

0 Comments