Maneno ya Bwana Yesu: “Leo niletee wanadamu wote kiujumla, hasa wakosefu wote. Uwazamishe ndani ya Bahari Kuu ya Huruma yangu. Kwa njia hii utatuliza uchungu wangu kwa ajili ya roho zilizopotea.”
Ee Yesu
mwenye Huruma kabisa, ambaye asili yako ni Huruma na Msamaha, usizitazame
dhambi zetu, bali utazame tumaini tulilo nalo katika wema wako usio na mwisho.
Utupokee sisi sote chini ya ulinzi wa Moyo wako wenye Huruma tele. Usimwache
hata mmoja. Tunakuomba hayo kwa njia ya upendo ule unaokuunganisha wewe na Baba
na Roho Mtakatifu, katika Umoja wa Utatu Mtakatifu, daima na milele. Amina.
Baba
yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …
Baba wa
Milele, uwatazame kwa macho ya huruma wanadamu wote, na hasa wakosefu maskini, waliongizwa
ndani ya Moyo wa Mwanao mpenzi, Bwana wetu Yesu Kristu, ulio na huruma yako
kuu, ili nasi tuisifu na kuitukuza tangu sasa na milele yote. Amina.
0 Comments