Dogma ya Kupalizwa Mbinguni inafundisha kwamba mwishoni mwa maisha yake duniani, Maria alichukuliwa—mwili na roho—kwenda mbinguni. Huko, anaketi upande wa kulia wa Mwana wake, akiwa Mfalme wa Mbinguni na Duniani. Misingi ya mafundisho haya inatokana na Maandiko. Kupalizwa Mbinguni ilitagazwa kama dogma iliyoelezwa ya Kanisa Katoliki mnamo 1950 na Papa Pius XII aliposema "Kwa mamlaka ya Bwana wetu Yesu Kristo, ya Mitume Watakatifu Petro na Paulo, na kwa mamlaka yetu wenyewe, sisi tunatangaza, na kuidhinisha kuwa ni dogma iliyofunuliwa kimungu: kwamba Mama Mtakatifu wa Mungu, Bikira Maria, akiisha kumaliza safari ya Maisha yake duniani, alichukuliwa mwili na roho katika utukufu wa mbinguni."
Katika
chapisho langu juu ya kukingiwa kwake Bikira Maria dhidi ya dhambi, Nimeeleza kuwa
Krsto alimheshimu mama yake kwa kumlinda dhidi ya dhambi tangu mwanzo wa maisha yake. Hiyo
ingekuwa heshima ya kutosha, lakini tunajua kwamba hakuishia hapo. Kama alivyopokea ukombozi kama matunda
ya kwanza ya kazi ya Kristo, vivyo hivyo alipokea ufufuo wa mwili na utukufu wa
mbinguni.
Ushahidi
wa maandiko juu ya kupalizwa kwake mbinguni unaweza kufuatiliwa hadi karne ya
nne. Kufikia mwishoni mwa karne ya sita, mafundisho na sikukuu yalikuwa tayari
yamekubalika kote Kanisani. Hakuna ushahidi wa kutosha kwamba mafundisho hayo
yalipingwa au kuhojiwa kwa dhati wakati huo wa Kanisa; wala kanisa wala jiji
lolote halijawahi kudai umiliki wa mabaki ya Bikira Maria. Hilo, peke yake, ni
jambo la kuvutia. Kanisa la mapema, miji, na makanisa vilishindania mabaki ya
mitume wakuu na mashahidi. Kama mabaki ya Maria yangelikuwa duniani,
yangelikuwa zawadi kubwa, na utafutaji na uhamishaji wa mabaki hayo kutoka jiji
hadi jiji ungekuwa na ushuhuda mzuri. Lakini tena, rekodi ya kihistoria
haionyeshi dalili hata moja ya kisanduku cha mabaki ya Maria—isipokuwa kaburi
lake tupu. (Na miji miwili inadai zawadi hiyo!).
Tunapata
taarifa ya tukio hilo kidogo zaidi iliyotulia kutoka kwa Mtakatifu Yohane wa
Damasko katika nakala ya barua aliyoihifadhi kutoka kwa Kiongozi mkuu wa
Yerusalemu wa karne ya 5 anayeitwa Juvenalius kwa Malkia Mzuri wa Byzantine
Pulcheria. Inaonekana Malkia alikuwa ameomba masalia ya Mama Mtakatifu Bikira
Maria. Juvenalius alijibu kwamba, kulingana na mapokeo ya zamani, mwili wa Mama
wa Mungu ulichukuliwa mbinguni baada ya kifo chake, na akastaajabu kwamba
Malkia hakuwa akiifahamu hii (akimaanisha kwamba ilibidi iwe maarufu katika
Kanisa wakati huo).
Juvenalius
aliambatanisha barua hii na taarifa ya jinsi mitume walivyoitwa kwa njia ya
miujiza kwa mazishi ya Mama wa Mungu, na jinsi baada ya kufika kwa mtume
Tomaso, kaburi lake lilifunguliwa, na mwili wake haukuwepo, na jinsi
ilifunuliwa kwa mitume kwamba alikuwa amechukuliwa mbinguni, mwili na roho.
Baadaye, karne ya 6, fundisho juu ya kupalizwa mbinguni lililindwa na Mtakatifu
Gregori wa Tours, na hakuna mtakatifu au mwanafalsafa wa Kanisa aliyepinga
imani hiyo baadaye.
Ni dhahiri,
vipande hivi vya ushahidi pekee havithibitishi kwamba mafundisho haya ni kweli.
Lakini Kanisa linaamini kwamba kutokana na kumwagika kwa Roho Mtakatifu katika
Pentekoste, watu wa Mungu kwa ujumla wanayo ile ambayo Mtakatifu Agustino na
Mtakatifu Tomaso wa Aquino waliiita affectio au inclinatio fidei. Yaani,
mwelekeo wa kihisia unaowavuta kwa ukweli wa imani. Kwa kuwa Roho Mtakatifu ni
Roho wa Kweli, makubaliano ya waamini kuhusu jambo la kweli la kiungu, na haswa
ya watakatifu (ambao wamejaa Roho Mtakatifu), hakika si jambo la kupuuzwa.
Pili,
inadaiwa kwamba hakuna maelezo ya kupalizwa kwake Bikira Maria katika Maandiko. Lakini ningedai (nikimfuata
msomi na mwalimu wa Kikatoliki anayeitwa Scott Hahn) kwamba kuna, mrejeo wa
mafumbo ya kupalizwa moja kwa moja katika sehemu tunayotarajia kuipata ikiwa
mafundisho yalikuwa kweli: yaani, katika maandishi ya Mtume Yohane, yule ambaye
Bwana alimkabidhi Mama yake saa ya kifo chake Msalabani, na haswa katika kitabu
ambacho labda ni cha mwisho katika Agano Jipya kuandikwa, kitabu cha Ufunuo.
Katika
kitabu chake kipya, kinachoitwa Hail Holy Queen, Profesa Hahn
anaonyesha kwa hakika kwamba hadithi ya Bikira Maria kumtembelea binamu yake Elizabeti katika Injili ya Luka,
sura ya kwanza, ina fanano nyingi na ya kushangaza na ya Agano la Kale ya Mfalme Daudi kuletewa
Sanduku la Agano hadi Yerusalemu katika 2Samweli 6.
Mfanano
huu haukuwa wa bahati mbaya: Yohane wa Damasko anatuambia, kwa njia yake ya kipekee, kwamba
Maria mwenyewe ni Sanduku jipya la Agano. Kama vile Sanduku katika Israeli ya
zamani lilikuwa na mbao za Amri za Mungu na baadhi ya mana ya mkate kutoka
mbinguni - ishara za Agano la Kale - hivyo tumbo la Maria lilikuwa na ishara ya
ahadi ya Agano Jipya na Mkate wa Kweli wa Uzima: Yesu Mwokozi wetu Mwenyewe.
Hivyo, ilikuwa tayari imani ya Kanisa la Mitume kwamba Maria alikuwa Sanduku
jipya la Agano.Sasa, Sanduku la Kale la Agano lilipotea kwa karne nyingi, na
Wayahudi wengi hawakujua mahali ambapo wangeweza kulipata (kwa kweli, bado
linaonekana kupotea mpaka leo).
Ikiwa
tunazingatia hili, sasa tutizame tunachokipata kwa kusoma mwishoni mwa sura ya 11 ya Kitabu cha Ufunuo:
“Ndipo
hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana
ndani ya hekalu lake, kulikuwa na umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi na
mvua kubwa”.
Wow,
ni onyesho la sauti na la kuonekana! Sanduku lilikuwa limepatikana! Lakini tunapoangalia
kitabu cha Ufunuo kinatuambia baadaye (na kumbuka: sehemu na sura za Biblia
si sehemu ya maandishi ya awali: ziliwekwa na wamonaki muda mrefu baadaye ili
kutusaidia kuona mistari ya Maandiko kwa urahisi zaidi, kwa hivyo sentensi
ifuatayo mwanzoni mwa sura ya 12 ilifuata moja kwa moja ile mwishoni mwa sura
ya 11 katika maandishi ya awali):
“Na
alama kubwa ikatokea mbinguni, mwanamke amevikwa jua, na mwezi chini ya miguu
yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili; alikuwa mjamzito...
[alimzaa mtoto wa kiume, yule atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma]”.
Dhahiri,
kile ambacho Yohane alionyeshwa katika maono yake, kilichorekodiwa hapa katika
Kitabu cha Ufunuo, ni kwamba Sanduku la Agano sasa liko mbinguni kama "mwanamke
amevikwa jua" ambaye mwana wake ni Masihi (atakayetawala kwa
"fimbo ya chuma," kulingana na Zaburi 2:9).
Hakika,
baadhi ya mababa wa Kanisa waliona kifungu hiki kama marejeo kwa Maria, Mama wa
Mwokozi wetu, ikiwa ni pamoja na Mtakatifu Ephrem, Mtakatifu Ambrose, na
Mtakatifu Agustino. Wakati huo huo, wengi wa Mababa waliona
"mwanamke" anayetajwa kama ishara ya Israeli, na Kanisa, Israeli
Mpya. Kuna hakika ishara kwamba hii pia ndio inayoonesha na ishara hapa (kwa
mfano, ana taji ya nyota kumi na mbili kichwani mwake, ikionesha kabila kumi na
mbili za Israeli, na mitume kumi na mbili).
Kwa hivyo ni tafsiri ipi sahihi? Zote mbili ni sahihi! (Na Mababa wa zamani hawakuona mgongano kati yao.) Haikuwa nadra katika fasihi ya Kiyahudi ya zamani kutumia mfano wa mara mbili: mtu halisi kutumika kama ishara ya kikundi kizima cha watu. Kwa mfano, ni kwa kiasi kikubwa kwamba kifungu maarufu katika Isaya 53 kuhusu mateso ya Masihi ("Alikuwa mwenye dhihaka na kupuuzwa na watu, mtu wa huzuni na kujua mateso," n.k.) pia ni ishara ya wito wa mateso wa watu wote wa Israeli.
Kwa
njia sawa, Maria, Mama wa Kanisa, inatumiwa katika kitabu cha Ufunuo
kuwakilisha utimilifu wa wito wa Israeli katika watu wa Mungu wapya, ambao
watabeba Kristo ulimwenguni. Si ajabu kwamba Kanisa lilipoanza kuandaa
maandishi ya liturujia kwa Sikukuu ya Kupalizwa Mbinguni, lilifanya uhusiano
(ulioanzishwa awali na baadhi ya Mababa wa zamani), kati ya Zaburi 131:8 na
siri ya mwanamke ambaye ni sanduku la mbinguni: "Simama, Bwana, ingia
mahali pako pa raha, Wewe na sanduku la nguvu zako." Baada ya Bwana
"kuinuka" kutoka kwa wafu, Alikwenda naye mbinguni pamoja na
"sanduku" halisi la Agano Jipya, mwili wa Mama yake Maria. Kwa kuwa
Wayahudi wa kale waliamini kwamba sanduku la asili lilifanywa kwa mbao
isiyoharibika, hivyo kifungu hiki kinatabiri kifo kisichoharibika alichopewa
Maria na Mwana wake aliyefufuka. Kristo
alileta sanduku la agano jipya yaani Bikira Maria kuishi katika patakatifu ndani ya hekalu la Yerusalemu ya mbinguni.
Hatimaye,
naamini Kupalizwa kwake Mbinguni Bikira Maria ni ukumbusho wa ukweli
wa kufufuka. Tunapata muono wa zawadi iliyoahidiwa na kifo na ufufuko wa Bwana
Yesu. Kama vile Yesu anavyosema katika Injili ya Yohane, "Katika nyumba
ya Baba yangu mna makao mengi. Naenda kuwaandalia mahali." Mama
wa Yesu amekwenda kwenye nyumba ya mbinguni. Lakini Maria ni Mama yetu pia! Je,
usingefikiri kwamba pale Mama yetu alipo, huko ndiko tutakakokuwa?
0 Comments