Maelezo
yafuatayo ni ufafanuzi wa masharti yaliyomo katika ombi la Bikira Maria huko
Fatima, Ureno kuhusu Komunio ya kulipia, siku ya Jumamosi ya kwanza ya mwezi
kwa miezi mitano mfululizo.
Ahadi iliyotolewa
na Bikira Maria kwa Lucia tarehe 13 Julai 1917, kwamba atamtokea baadaye kumuelezea kuhusu Ibada ya Jumamosi Tano za Kwanza za miezi,
ilitekelezwa tarehe 10 Desemba 1925. Lucia wakati huo alikuwa Mnovisi katika Wamonaki wa Dorothean huko
Tuy, Hispania. Wakati huu, Bikira Maria alimtokea akiwa pamoja na Mtoto Yesu, mtoto Yesu alianza kusema kwanza kwa Lucia:
“Kuwa
na huruma kwa Moyo wa Mama yako
Mtakatifu, uliofunikwa na miiba ambayo watu wasio na shukrani wanaiweka ndani
yake kila wakati, wakati hakuna mtu anayelipia ili kuondoa miiba hiyo kwake."
Kisha
Bikira Maria akamwambia Lucia kama ifuatavyo:
“Tazama,
binti yangu, Moyo wangu uliozungukwa na miiba, ambayo watu wasio na shukrani
wanaichoma kila wakati kwa matukio yao
ya kumkufuru na kutokushukuru. Nipe faraja, wewe angalau; na fanya inayowezekana
kujulikana kwa niaba yangu kwamba ninahidi kusaidia saa ya kufa, na kuwapa neema zinazohitajika kwa wokovu, wote
wanaotubu dhambi zao siku ya Jumamosi ya
kwanza ya miezi mitano mfululizo, kupokea Komunyo Takatifu, kusali mafungu
matano ya Rozari, na kutafakari kwa
dakika kumi na tano juu ya mafumbo ya Rozari, kwa kusudi la kulipia moyo wangu
usio na doa.”
KWA
NINI JUMAMOSI TANO?
Mara
kwa mara watu huuliza kwa nini Bikira Maria aliomba Komunio za kulipia Jumamosi
tano za kwanza, badala ya idadi nyingine. Bwana wetu alijibu swali hilo alipotokea tena kwa Sr.
Lucia Mei 29, 1930. Alifafanua kuwa ilikuwa kutokana na aina tano za makosa na
makufuru dhidi ya Moyo Mtakatifu wa Bikira Maria, yaani:
(a)
Kufuru dhidi ya kukingiwa kwake dhambi ya asili,
(b)
Kufuru dhidi ya ubikira wake,
(c)
kumkufuru dhidi ya kuitwa Mama wa Mungu,
(d)
kufuru kwa
kukataa na kukashifu picha zake, na
(e)
Uzembe wa kupanda katika mioyo ya watoto ujuzi na
upendo wa Mama huyu Mtakatifu.
Roho
ya kulipia ni hamu ya upendo wa kufidia na kufariji Moyo wenye Huzuni na
Mtakatifu wa Mama yetu. Inazingatia makosa ambayo Moyo Mtakatifu wa Maria
anapokea sasa kutoka kwa wale wanaokataa msaada wake wa kimama na kudharau sifa
zake. Mtu anapaswa kuweka nia hii kabla ya kutekeleza maombi ya Bikira Maria
juu ya ibada hii ya Jumamosi ya kwanza ya mwezi. Kubadilisha nia halisi wakati
wa kutekeleza ni bora zaidi.
MAMBO
YA KUFANYA KWA JUMAMOSI YA KWANZA YA MWEZI KWA AJILI YA IBADA HII.
1. MAUNGAMO.
Tarehe
15 Februari 1926, Mtoto Yesu mwenyewe alikuja kumtembelea Sr. Lucia pekee na
kuuliza ikiwa ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Maria ilikuwa inasambazwa. Sr. Lucia
alizungumzia ugumu ambao baadhi ya watu wanapata katika kutubu Jumamosi ya
kwanza, na aliuliza ikiwa wanaweza kupewa siku nane ili kutimiza ombi la Bikira
Maria. Yesu alijibu: "Ndiyo, hata zaidi ya wakati huo, mradi watu hao
wanipokee wakiwa katika neema na wakiwa na nia ya kulipia Moyo Mtakatifu wa
Maria."
Kutubu:
Toba na Kugeuka: Ili kutimiza mahitaji haya kwa njia inayofaa kabisa, lazima
tuangalie zaidi ya umbo la kwenda kutubu wakati uliopangwa, kuelekea roho ya
kweli ya toba na huzuni ya kudumu kwa dhambi zetu. Roho hii ya kutubu inapaswa
kuvamia maisha yetu yote, kwa njia ambayo inatulazimisha kutembea daima katika
njia ya kubadilika kwa maisha ambayo Bikira Maria aliomba. Katika kila ibada ya
kweli kwa Bikira Maria - na ibada kwa Moyo wake Mtakatifu ni kielelezo kamili
cha ibada hii ya kweli - lazima iwe na toba inayofaa, yaani, kurudisha mioyo
yetu kwa Kristo Mwokozi wetu. Kwa sisi sote (wote wenye dhambi), hii ni wito wa
kutubu kwa njia ya neema na kutii Mapenzi matakatifu ya Mungu. Hata kwa roho
zile ambazo tayari kwa kawaida huishi katika neema ya Mungu, ibada ya kweli kwa
Bikira Maria inawalazimisha zaidi na zaidi kufuata njia ya utakatifu, kwa
kujitahidi kujisafisha kila siku na yote yasiyo ya Mungu. Na ni hii ibada ya
kweli, ikitegemea kama ilivyo kwa toba ya kweli na kugeuka, inayowaumbia roho
halisi ya Utume wa Kikristo - hamu ya kuwaongoza wengine kwenye njia ile ile
kuelekea Moyo wa Mungu.
Ikiwa
mtu hawezi kutubu Jumamosi ya kwanza ya mwezi, anaweza kutubu ndani ya siku
nane. Hata kutubu kila mwezi kunaweza
kutosha, na haja ya kutimiza nia ya kulipia Moyo Mtakatifu wa Maria.
2.
KUPOKEA KOMUNYO TAKATIFU
3. KUSALI
ROZARI KWA IBADA NA KUTAFAKARI
"Kaa
nami kwa dakika kumi na tano huku unatafakari juu ya mafumbo ya Rozari."
Swali
mara nyingi hulizwa: Je! Kutafakari wakati wa kusali Rozari kunatimiza hali
hii, au kuna hitaji la dakika kumi na tano ya ziada ya kutafakari mbali na
kusali rozari? Hivi karibuni, Sr. Lucia wa Fatima alithibitisha kuwa
inahitajika dakika 15 zaidi ya kutafakari.
Kuingizwa
mwisho katika muktadha wa Fatima, iliyochapishwa kwenye Kalenda rasmi ya Mahali
Patakatifu kwa mwaka wa 1940, na kusainiwa na Dom Jose Correia da Silva, Askofu
wa kwanza wa Fatima, ilitoa muhtasari wa maombi ya Bikira Maria kuhusu Jumamosi
Tano za Kwanza. Kutoka kwenye taarifa rasmi katika Kalenda ya Mahali
Patakatifu, tunasoma orodha ya Askofu inayohusiana na ibada ya Jumamosi tano:
Inahusisha
kwenda kutubu, kupokea Komunyo, kusali mafungu matano ya Rozari, na kutafakari kwa
robo saa juu ya fumbo la Rozari siku ya kwanza ya Jumamosi kwa miezi mitano
mfululizo. Kutubu inaweza kufanywa siku nane kabla au baada ya Jumamosi ya
kwanza ya kila mwezi, mradi Komunyo Takatifu ipokelewe katika neema. Ikiwa mtu
atasahau kuunda nia ya kulipia Moyo Mtakatifu wa Maria, inaweza kuundwa wakati
wa Kutubu inayofuata, kwa kutumia fursa ya kutubu wakati wa fursa ya kwanza.
Tafakari
inajumuisha fumbo moja au zaidi; inaweza hata kujumuisha yote, pamoja au kando,
kulingana na mvuto au ibada binafsi; lakini ni bora kutafakari fumbo moja kila
mwezi.
Akizungumzia
mahitaji ya "kaa nami kwa dakika kumi na tano wakati unatafakari juu ya
fumbo la Rozari," maoni ya Askofu da Silva kwamba "ni bora
kutafakari fumbo moja kila mwezi" inaweza kutumika tu kwa dakika 15
ziada, kwa kila mafungu ya Rozari lazima iwe na tafakari yake ya pekee.
Kama
ilivyo kwa Rozari, tafakari hii inaweza kufanywa wakati wowote au mahali wakati
wa Jumamosi ya kwanza. Tena, kama Rozari, wakati na mahali pazuri ingekuwa
mbele ya Ekaristi Takatifu kabla au baada ya Misa
4. KWA
NIA YA KULIPIA.
Hali
zote zilizotajwa hapo juu - kuanzia namba 1 hadi 3 - zinapaswa kutimizwa kwa
nia ya kulipia Moyo Mtakatifu wa Maria. Wakati
Mtoto Yesu alipomtebelea Sr.
Lucia (Februari 16, 1926), alimuuliza: "Yesu wangu, wale wanaosahau
kuunda nia, vipi?" Yesu alijibu: "Wanaweza kufanya hivyo
katika maungamo yao yanayofuata, wakitumia fursa yao ya kwanza kwenda
kutubu."
Haya
ni mahitaji ya chini ya kutimiza hali ya ahadi ya Bikira Maria ya kupata "saa
ya kufa neema zinazohitajika kwa wokovu." Hata hivyo, hizi Komunyo za
kulipia , kama ilivyoelezwa, ni sehemu tu ya ibada ya Moyo Mtakatifu wa Maria.
Ahadi
zinazohusiana na Ibada ya Jumamosi Tano za Kwanza.
1.
Wokovu wa roho zetu
Kwa
wote wanaotimiza masharti yote yaliyotolewa, siku ya kwanza ya Jumamosi kwa
miezi mitano mfululizo “... ninaahidi kuwasaidia saa ya kufa na neema zote
zinazohitajika kwa wokovu wa roho yao”. Ibada hii ndogo iliyoanzishwa kwa
moyo mzuri, basi, ni ya kutosha kutupatia, kwa uhakika kama ilivyo na
Sakramenti, neema ya kudumu hadi mwisho, ya wokovu wa milele! Na ahadi hii
haina kizuizi, kikwazo, au kikomo. “Kwa wote wanaotimiza... Ninaahidi.
Mbingu milele kwa Komunyo Takatifu tano!”
2.
Wokovu wa wenye dhambi
“Roho
nyingi zinapata hukumu ya haki ya Mungu,
kwa dhambi zilizofanywa dhidi yangu,
Jitolee kwa nia hii na Sali”. (Bikira Maria kwa Sr. Lucy huko
Tuy, Juni 13, 1929.) Kwa kuzingatia ibada hii ndogo, Wao (Yesu na Maria)
wanataka kutoa neema ya msamaha kwa roho ambazo zimekuwa na bahati mbaya ya kuukosea
Moyo Mtakatifu wa Maria, kama aliandika
Sr. Lucy katika barua ya Mei, 1930.
3.
Amani duniani
“Ikiwa
dunia itakuwa na vita au amani inategemea na ibada hii, pamoja na kuwekwa wakfu kwa Russia kwa Moyo Mtakatifu wa Maria. Ndio
maana nataka ienezwe kwa shauku, hasa kwa sababu hii pia ni mapenzi ya Mama
yetu wa Mbinguni.” Sr. Lucy, Machi 19, 1939.
0 Comments