Jina la Maria, MAMA
WA MUNGU, ni mojawapo ya majina ya zamani na yanayotumiwa mara kwa mara kwa
Maria, wakristo wamekuwa wakiitumia jina
ili tangu karne za mwanzo za kanisa. Na hali hii Ya kuwa Mama wa Mungu
inafahamika sana hasa kwa jina la kigiriki “Theotokos”. Wakristu wa
kwanza walimuita Maria, Mama wa Mungu
bila kusita, kulikuwa na mfano wa maandiko na maandiko hayo yalionekana kuwa na
mantiki. Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, na Maria alikuwa mama yake, basi hilo
lilimfanya awe Mama wa Mungu.
Katika karne ya tano
hata hivyo, baadhi ya wakristu walileta
pingamizi sawa na pingamizi linaloonekana kuwepo mpaka leo kwa wasio
wakatoliki, walidai kwamba jina MAMA WA MUNGU lilimaanisha kwamba Maria
alikuwa “chanzo cha Mungu”. Wapingaji hao walisema wanaweza kukubali jina “Mama
wa Kristu” lakini sio “Mama wa Mungu”. Walidai Maria alizaa tu asili ya kibinadamu ya
Kristo, sio asili ya kimungu ya Kristo.. Kanisa likiongozwa na Papa Celestine I
na Mtakatifu Cyril wa Alexandria, lilipinga. Kama vile Mt. Cyril alivyosema “Mama
anazaa mtu, sio asili”. Kulingana na
hivyo, Maria alizaa Yesu Kristu, ambaye alikuwa na ni nafsi ya kimungu.
Ingawa Maria hakumleta Mungu mwanzo au kumzalisha, lakini alimchukua tumboni
mwake na kumzaa, alikuwa MAMA WA MUNGU.
Mgogoro kuhusu
cheo cha Maria kama Mama wa Mungu, ulishughulikiwa mwaka 431 B.K, katika Mtaguso
wa Efeso. Katika mtaguso huo kulikuwa na
mambo mengi zaidi ya kuongelea kuliko kutetea tu cheo cha Maria, suala kuu
lilikuwa fundisho la kikristo kuhusu asili mbili za kristu. Kanisa lilikuwa na lengo la kutatua swali moja. Je, Yesu
alikuwa mtu mmoja au wawili? Kwa kukataa fundisho la mzushi Nestorius, kanisa
lilikiri kwamba Yesu ni mtu mmoja wa
kimungu, mwenye asili mbili – asili yake ya kibinadamu kutoka kwa mama yake na
asili yake ya kimungu kutoka kwa Mungu Baba.
Maria hakumpa Yesu asili yake ya kimungu au utu wake wa
kimungu – mambo ambayo alikuwa nayo milele kama mwana wa pekee wa Baba. Maria
alimzaa Yesu kama mtu mzima alimzaa Yesu Kristo akiwa na asili ya kimungu na ya
kibinadamu. Hicho ndicho tunachokiri kila mara tunaposali Kanuni ya Imani.
Kumuita Maria
Mama wa Mungu kunathibitisha ukweli ambao lazima usemwe ili kulinda ukweli
muhimu kuhusu Kristo. Maria ni kiungo kati ya utu na Umungu wa mwana wake. Yeye
ni ishara kwamba Yesu ni Mungu-Mtu.
0 Comments