Baada ya Sadaka ya
Misa Takatifu,
Rozari Takatifu ni sala inayompendeza zaidi Bikira Maria. Akivaa taji ya Mbinguni na kuketi
karibu na Mfalme, mwanawe mpendwa, Bikira Maria amepewa idhini ya kutoa neema
za Mungu kwa watoto wake wa kiroho, kwa niaba ya ambao yeye daima anawaombea.
Bikira Maria aliahidi
Mtakatifu Dominiko na wote wanaomfuata kwamba "Cho chote utakachokiomba kwa njia ya Rozari
kitatolewa." Pia alimfunulia ahadi 15 maalum kwa wale wanaosali Rozari kwa
uaminifu, ahadi hizo ni
kama ifuatavyo;
1. Kila anayenitumikia kwa
kusali Rozari atapokea neema maalumu.
2. Ninakuhakikishia ulinzi
wangu maalumu
na neema kubwa kwa wote wanaosali Rozari.
3. Rozari itakuwa kinga yenye
nguvu dhidi ya jehanamu, itaharibu uovu, kupunguza dhambi, na kushinda uzushi.
4. Italeta mafanikio ya kazi
nzuri; itapata kwa roho rehema nyingi za Mungu; itaondoa mioyo ya watu kutoka
upendo wa dunia na vitu vyake vya ubatili na kuwaelekeza kwa mambo ya Milele.
Oh, roho zingetakasika kwa njia hii!
5. Nafsi inayojitolea kwangu
kwa kusali Rozari haitapotea.
6. Kila anayesali Rozari kwa
unyenyekevu, akijitahidi kutafakari Mafumbo yake Matakatifu, hataweza
kupatwa na bahati mbaya.
Mungu hatamrudi kwa haki yake; hataangamia kwa kifo kisichotarajiwa; ikiwa ni
mwadilifu ataendelea kuwa katika neema ya Mungu na kuwa wa kustahili Maisha ya
Milele.
7. Kila anayeonyesha kweli kwa
Rozari hatakufa bila Sakramenti za Kanisa.
8. Wanaofuata kwa uaminifu
kusali Rozari watakuwa na Nuru ya Mungu na wingi wa Neema Zake maishani mwao na
wakati wa kifo wataushiriki utukufu wa Watakatifu wa Mbinguni.
9. Nitawaokoa kutoka Toharani wale wanaojitolea kwa Rozari.
10. Watoto waaminifu wa Rozari
watastahili cheo cha juu cha Utukufu mbinguni.
11. Utapata yote utakayoniomba
kwangu kwa kusali Rozari.
12. Wote wanaosambaza Rozari
Takatifu watasaidiwa
na mimi katika mahitaji yao.
13. Nimepata kutoka kwa
Mwanangu wa Kimungu kwamba wote wanaotetea Rozari watakuwa na msaada wa Jeshi
zima la Mbinguni wakati wa maisha yao na saa ya kufa.
14. Wote wanaosali Rozari ni
Watoto wangu, na ndugu wa Mwanangu pekee Yesu Kristo.
15. Ibada kwa Rozari yangu ni
ishara kubwa ya kuchaguliwa mapema.
Ni ajabu kushuhudia neema na
amani tunayopokea kupitia kitendo cha kusali Rozari. Kutenga muda wa kusali
Rozari — pekee, pamoja na familia, au na marafiki — ni tendo dogo la imani
linaloleta thawabu kubwa. Na kama Sister Lucia dos Santos, mmoja wa watoto
ambaye Bikira Maria alimtokea huko Fatima, alivyosema, "Hakuna tatizo,
lolote jinsi lilivyo gumu... ambalo halitaweza kutatuliwa na sala ya Rozari
Takatifu."
0 Comments