Mnamo majira
ya saa sita usiku, Mtakatifu Catherine Labouré aliamshwa na sauti laini,
ikisema, "Sista,sista, sista." Matukio ya kimiujiza yalimpeleka
kwenye kikanisa ambapo Bikira Maria alitokea na kuketi karibu na Altare ya
kikanisa hicho. Mtakatifu Catherine alipiga magoti miguuni pake, akaweka mikono
yake mikononi mwa Maria, akamtazama machoni, na kufanya mazungumzo ya moyo kwa
moyo naye.
Miezi
minne baadaye, mwezi wa Novemba mwaka 1830, Maria alitokea tena kwa Mtakatifu
Catherine katika Kikanisa hicho kilichochopo Rue de Bac. Wakati huu, Mama yetu
Mtakatifu alikuwa amesimama juu ya duara, na miali ya mwanga wa kung'aa ikitoka
kwenye mikono yake iliyotandazwa. Karibu na Mama Mara kulikuwa na maandishi: "Ee
Maria, Mkingiwa dhambi ya asili, utuombee sisi tunakuomba." Maria
aliposema na Mtakatifu Catherine, alisema, "Tengenezeni medali kwa mfano huu.
Wale wanaoivaa watapokea neema kubwa, hasa wakiivaa shingoni. Wale wanaoisoma
sala hii kwa unyenyekevu watakuwa, kwa njia ya pekee, chini ya ulinzi wa Mama
wa Mungu. Neema zitamiminika kwa wingi kwa wale wanao amini."
Kwa
idhini ya Kanisa Katoliki, medali za kwanza zilitengenezwa mwaka 1832 na
kusambazwa Paris, nchini Ufaransa. Inajulikana kuwa medali kumi za awali zipo,
na mojawapo inahifadhiwa kwenye Shrine la Medali ya Miujiza.
Kwa
haraka zaidi, baraka ambazo Maria aliahidi zilianza kuonekana kwa wale
waliokuwa wakivaa medali yake, na hivi Ufaransa yote watu walianza kuita medali
huo "Medali wa Miujiza." Matumizi ya Medali yalisambaa kutoka
nchi hadi nchi, na wakati wa kifo cha Mtakatifu Catherine mwaka 1876, medali
zaidi ya bilioni moja zilikuwa zimetengenezwa. Mpaka Leo, Medali bado inavuta
baraka kutoka kwa Mungu kwa mwili na roho.
MAANA
YA MEDALI YA MIUJIZA.
Medali ya Miujiza awali ilijulikana kama Medali ya Bikira Maria Mkngiwa dhambi ya asili, lakini, kutokana na miujiza mingi kutoka kwa wale waliokuwa wakivaa, watu walianza kuipa jina la Medali ya Miujiza, na jina likabaki. Medali hii ni kumbukumbu ya kuona ya wokovu wetu kupitia Yesu Kristo.
Upande
Wa Mbele.
Upande
wa mbele wa Medali ya Miujiza unaonyesha Maria Mkingiwa dhambi ya asili, mikono
yake ikiwa wazi, imejaa mwanga. Mtakatifu Catherine Labouré alimwona Bikira
Maria akionekana hivi na kumsikia akisema, "Tengenezeni medali
kufuatana na mfano huu. Kila mtu atakayevaa shingoni atapokea neema
kubwa." Maria anasimama juu ya duara kama Malkia wa Mbingu na Dunia.
Miguu yake inaonekana ikiwa imekanyaga nyoka kuashiria kwamba Shetani na wafuasi wake
wote ni dhaifu mbele zake (Mwa. 3:15). Kumbukumbu ya "Bikira Maria kuumbwa
bila dhambi" inaunga mkono dogma ya Kukingiwa kwake Bikira Maria dhidi ya
dhambi — Dogma hii inamuelezea Maria kuwa “asiye na dhambi”, "amejaa neema,"
na "amebarikiwa miongoni mwa wanawake wote" (Lk. 1:28). Dogma ya Bikira
Maria kukingiwa dhambi ya asili ilitangazwa miaka 24 baadaye mwaka 1854, na
kuthibitishwa wakati Maria alipotokea kwa Mtakatifu Bernadette Soubirous huko
Lourdes, Ufaransa, mwaka 1858.
Upande
Wa Nyuma.
Kwenye
upande wa nyuma, Msalaba na herufi M zinaashiria uhusiano wa karibu wa Maria na
mateso, na kifo cha Mwana wake. Msalaba unaweza kuashiria Kristo na ukombozi
wetu, na mstari chini ya msalaba ni ishara ya ardhi na Altare, kwa sababu ni
kwenye Altare wakati wa Misa kwamba sadaka ya Kalvari inaendelea kuwepo duniani
leo. M inamaanisha "Maria" na "Mama." Uunganishaji wa
herufi za mwanzo za Maria na msalaba unaonyesha ushiriki wa karibu wa Maria na
Yesu na ulimwengu wetu. Hapa, tunaona jukumu la Maria katika wokovu wetu na
jukumu lake kama Mama wa Kanisa.
Chini
ya Msalaba, mstari, na M kuna mioyo miwili iliyoko upande mmoja: Moyo Mtakatifu
wa Yesu uliovikwa miiba na Moyo Immakulata wa Maria uliopenywa na upanga. Mioyo
miwili inawakilisha upendo wa Yesu na Maria kwetu.
Nyota
kumi na mbili zinaashiria kabila kumi na mbili za Israeli na mitume kumi na
mbili, wanaowakilisha Kanisa lote wanavyomzunguka Maria. Pia inakumbusha maono
ya Mtakatifu Yohane, mwandishi wa Kitabu cha Ufunuo (12:1), ambapo "ishara
kubwa ikaonekana mbinguni, mwanamke amevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake,
na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili."
Karibu
kuvaa Medali ya Miujiza, alama ya neema na ulinzi kutoka kwa Bikira Maria.
Medali hii ni kumbukumbu ya upendo wa Yesu na Maria kwetu na ni chanzo cha
baraka tele. Kama vile Mtakatifu Catherine Labouré alivyoagizwa na Bikira
Maria, kuvaa medali hii ni kujitia chini ya ulinzi wa Mama wa Mungu na kupokea
neema kubwa. Kwa mujibu wa ahadi ya Maria, wale wanaoivaa watapata ulinzi
maalumu na baraka tele. Jiunge nasi katika kuvaa Medali ya Miujiza, kuwa karibu
na neema zinazotokana na upendo wa Mungu kupitia Bikira Maria.
0 Comments