Bernadette Subiri alizaliwa
mwaka 1844, mtoto wa kwanza wa Baba aliekuwa anafanya kazi za kusaga nafaka mwenye
umaskini mkubwa katika mji wa Lurdi kusini mwa Ufaransa. Familia ilikuwa
ikiishi katika chumba cha chini kabisa cha jengo lililoporomoka.
Tarehe 11 Februari 1858,
Bikira Maria alimtokea Bernadette katika pango juu ya kando za Mto Gave karibu
na Lurdi. Bernadette, katiak wakati huu alikuwa na umri wa miaka 14,
alijulikana kama msichana mwenye fadhila ingawa mwanafunzi dhaifu ambaye hata
hakuwa amepokea Komunyo yake ya kwanza. Akiwa na afya duni, alikuwa akiugua
pumu tangu akiwa mdogo.
Bikira Maria alimtokea
Bernadetta mara 18, tokeo la mwisho lilitokea katika sikukuu ya Bikira Maria wa
Mlima Karmeli, Julai 16. Ingawa ripoti za awali za Bernadette zilizua shaka, matokeo
hayo yalileta umati mkubwa wa watu wenye mshangao. Bernadette alieleza,kuwa
Bikira Maria alimwagiza kujenga kanisa katika eneo hilo alilomtokea. Watu
walikuwa wanakuja kujisafisha na kunywa maji ya chemchemi iliyokuwa imeanza
kujitokeza mahali ambapo Bernadette alikuwa ameagizwa kuchimba.
Kulingana na Bernadette, Bikira
Maria alipomtokea alikuwa msichana wa miaka 16 au 17 ambaye alikuwa amevaa joho
jeupe lenye mkanda wa buluu. Miguu yake ilifunikwa na maua ya njano, Rozari
ndefu ilikuwa mkono wake wa kulia. Bikira Maria alipotokea tarehe 25 Machi 1858
alimwambia Bernadette, "Mimi ni
Mkingiwa dhambi ya asili”.
Matokeo machache yamepitia
uchunguzi kama matokeo haya ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili. Lurdi
mpaka leo imekuwa ni moja ya sehemu maarufu zaidi ulimwenguni, ikivutia
mamilioni ya wageni. Miujiza mingi imekuwa ikifanyika huko Lurdi na katika maji
ya chemichemi yaliyopo huko wengi wemeponywa. Baada ya uchunguzi wa kina,
mamlaka ya Kanisa ilithibitisha uhalali wa matokeo hayo mwaka 1862.
Wakati wa maisha yake,
Bernadette aliteseka sana. Aliandamwa na umma pamoja na maafisa wa serikali
hadi hatimaye alilindwa kwa kupelekwa katika nyumba ya watawa. Miaka mitano
baadaye, aliomba kuingia katika Shirika la Masista wa Notre Dame wa Nevers.
Baada ya kipindi cha ugonjwa alisafari kutoka Lurdi na kuanza unovisi. Lakini
ndani ya miezi minne baada ya kufika, aliruhusiwa kuweka nadhiri zake. Alipona
na kuwa msaidizi wa wagonjwa na kisha kufanya
kazi sakristia, lakini matatizo ya kiafya yaliendelea kumsumbua. Aliaga dunia
tarehe 16 Aprili 1879, akiwa na umri wa miaka 35. Bernadette Soubirous
alitangazwa kuwa mtakatifu mwaka 1933.
Hapa kuna masomo ambayo kama
Watoto wa Maria tunaweza kujifunza kutoka kwa hadithi ya Mtakatifu Bernadette:
1. Kuwa na UJASIRI
Katika umri mdogo wa miaka 14, Mtakatifu Bernadette alikuwa na ujasiri wa matokeo ya Bikira Maria aliyejitambulisha kama “Mkingiwa dhambi ya asili”. Hii ilisaidia dogma ya Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya asili, ambayo ilitangazwa na Papa Pius IX miaka 4 tu kabla ya maono ya Mtakatifu Bernadette. Nasi ni wakati je sisi jasiri katika kutangaza na kueneza Ibada kwa mama huyu Bikira Maria au tunaogopa maneno ya watu?
Katika umri mdogo wa miaka 14, Mtakatifu Bernadette alikuwa na ujasiri wa matokeo ya Bikira Maria aliyejitambulisha kama “Mkingiwa dhambi ya asili”. Hii ilisaidia dogma ya Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya asili, ambayo ilitangazwa na Papa Pius IX miaka 4 tu kabla ya maono ya Mtakatifu Bernadette. Nasi ni wakati je sisi jasiri katika kutangaza na kueneza Ibada kwa mama huyu Bikira Maria au tunaogopa maneno ya watu?
2. Kuwa MTII
Licha ya matatizo yake yote ya kiafya, akiwa mtoto dhaifu na mgonjwa (alipata kipindupindu akiwa mdogo na pumu maisha yake yote), alifuata maagizo ya Mama yetu Bikira Maria kipindi chote cha matokeo ya Bikira Maria. Alisema “ndiyo” wakati Bikira Maria alipomwomba kwenda kwenye Grotto kwa muda wa wiki mbili; alisali Rosari pamoja naye; alipiga busu chini kama ishara ya toba kwa wenye dhambi; hakukataa kunywa maji ya chemichemi ingawa alikuta maji yenye matope kidogo; alikula mimea yenye uchungu karibu na chemchemi; alitoa maagizo ya Bikira Maria hasa kuoma Kanisa kujengwa huko. Leo, takriban mahujaji milioni 8 huzuru Madhabahu ya Bikira Maria wa Lurdi. Je, tujiulize nasi tunaitikia wito wa mama wa Mungu katika Maisha yetu hasa nyakati za shida? Au tunasubiri wakati wa Raha tu?.
3. Kuwa MNYENYEKEVU
Licha ya matukio na miujiza mingi iliyofanyika alijiona kama chombo tu na hakuona kustahili kwa lolote. Alijificha kutoka kwa ulimwengu na kuweka mambo yote kuwa ni ya kwake Bikira Maria na ujumbe wake.
4. Ishi maisha ya MAOMBI na TOBA
Katika barua yake kwa Papa Pius IX, Mtakatifu Bernadette anasema, "Silaha zangu ni maombi na toba, ambazo nitashika kwa nguvu hadi pumzi yangu ya mwisho." Alitumia maisha yake kwa kazi ya maombi, kusali kwa wenye dhambi kama Mama yetu alivyoagiza, na kujitolea kwa wagonjwa, licha ya ugonjwa na matatizo yake mwenyewe.
5. Ishi maisha ya IMANI
0 Comments