Maneno
ya Mwokozi: “Leo niletee roho za wale waliofungwa bado toharani, na uwazamishe
ndani ya Bahari Kuu ya Huruma yangu. Humo, mafuriko ya Damu yangu, yazimishe
miali ya motto mkubwa unaowachoma. Roho hizi zote hupendwa sana nami. Wako humo toharani kwa ajili ya kulipia Haki
yangu waliyoikosa hapa duniani. Wewe una uwezo wa kuwapatia faraja. Chota
rehema zote za Kanisa langu na uzitolee kwa ajili yao. Ungalijua tu ukali wa
mateso yao, loo! Ungetolea daima sadaka za kiroho kwa ajili yao, na kulipa deni
zima la Haki ya Mungu”.
Tuwaombee
marehemu wa toharani, wanaoilipia Haki ya Mungu, ili mtiririko wa Huruma wa
Damu ya Yesu uweze kupunguza na kufupisha mateso yao.
Ee Yesu
mwenye Huruma uliyesema, “Muwe na Huruma kama Baba yenu wa mbinguni alivyo na
Huruma”. Uzitazame kwa Huruma roho zile zinazoteswa toharani, kwa kulipia deni
la Haki ya Mungu waliyoikosea. Mtiririko ule wa Damu na Maji uliotoka kwa kasi
Moyoni mwako, uzimishe miale ya moto mkali wa toharani, ili huko pia Huruma
yako isifiwe na kuadhimishwa. Amina.
Baba
yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …
Baba wa
Milele, uzitazame kwa wema na huruma, roho zile zinazoteswa Toharani, wao pia
wameingizwa ndani ya Moyo wa Mwanao Mpenzi Yesu, na uchungu wote ulioelemea
Moyo na Roho yake, onyesha Huruma yako kwa roho zilizotiwa nguvuni na Haki
yako. Uwatazame watu hao kwa njia ya Madonda yake Yesu Mwanao Mpenzi, kwa kuwa
tunaamini kabisa kuwa wema na Huruma yako havina mwisho. Amina
0 Comments