Maneno ya Bwana Yesu: “Leo niletee wale wote wasioniamini na wale wasionijua bado. Wao pia niliwafikiria wakati wa mateso yangu makali, na juhudi watakayokuwa nayo baadaye ilinituliza Moyo wangu. Uwaingize katika Bahari Kuu ya Huruma Yangu.”
Tuwaombee
watu wote wasiomwamini Kristu, pamoja na wale wasiomjua bado.
Ee Yesu
mwema, Wewe ni Mwanga wa dunia nzima, uzipokee katika makao ya Moyo wako wenye
huruma sana, roho za wale wote wasiokuamini na wale wasiokujua bado. Achia
mionzi ya neema yako iwaangazie, ili nao pia pamoja nasi sote. Waweze kuitukuza
huruma yako ya ajabu, na usiwaache wakatoroka makao hayo, ambayo ni Moyo wako uliojaa
huruma. Amina.
Baba yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …
Baba wa
Milele, elekeza macho yako yenye huruma, kwa roho za watu wale wasiomwamini
Mwanao, na za wale ambao hawajakujua Wewe bado, ambao tumewaingiza ndani ya
Moyo wa Yesu uliojaa huruma tele. Uwavute kwenye mwanga wa Injili, watu hawa
hawajui Ukuu wa furaha iliyopo katika kukupenda Wewe. Uwajalie nao pia waweze
kuitukuza hisani ya huruma yako, kwa miaka isiyo na mwisho. Amin
0 Comments