Maneno
ya Mwokozi: “Leo niletee roho za wale ambao kwa namna ya pekee huiheshimu na
kuitukuza Huruma yangu, na uwazamishe ndani ya Huruma Yangu. Roho hizi ndizo
zilizonisikitikia zaidi wakati wa mateso yangu na kuipenya kabisa roho yangu.
Hawa ndio vielelezo na sura halisi ya Moyo wangu wenye Huruma na Wema. Roho
hizi zitakuja kung’aa kwa namna ya pekee katika maisha ya milele ijayo. Hakuna
hata mmoja kati yao atakayetupwa katika moto wa milele. Mimi Mwenyewe
nitamkinga kwa namna ya pekee kila mmoja wao saa ile ya kufa kwao”.
Tuziombee
roho za wale wanaoiheshimu kwa namna ya pekee Huruma ya Mungu, na kwa njia hii
huwa sura hai za Moyo wa Yesu ulio na Huruma nyingi.
Ee Yesu
mwenye Huruma, mwenye Moyo ulio Huruma yenyewe, uzipokee ndani ya Moyo wako
wenye Huruma sana, roho za watu wale wanaoiheshimu na kuitukuza kwa namna ya
pekee Ukuu wa Huruma yako. Roho hizi hushinda kwa nguvu ya Mungu mwenyewe.
Hukazana kihodari, hata katikati ya taabu na dhiki za kila aina, wakiitumainia
tu Huruma Yako, na kwa kujiunga nawe, ee Yesu, huwabeba wanadamu wote mabegani
mwako. Watu hawa hutamani kushiriki Msalaba wako kwa ajili ya wokovu wa watu
wote. Uzidi kuwafunika kwa Huruma yako daima na uwajalie fadhila za uvumilivu,
udumifu na nguvu za kuyasubiri yote. Amina.
Baba
yetu,…Salamu Maria … Atukuzwe, …
Baba wa
Milele, uzitazame kwa macho ya Huruma, roho wa watu wale ambao kwa juhudi na
upendo wa pekee, huitukuza na kuiheshimu Huruma yako isiyo na mipaka, ambao
wameingizwa ndani ya Moyo wa Yesu ulio na Huruma tele. Watu hawa ni kama Injili
iliyo hai. Wanakutukuza kwa maneno na matendo yao, na kwa kukuiga Wewe,
huwatendea watu wenzao kwa wema na huruma. Tunakuomba uwaonyeshe Huruma yako
Kuu zaidi na zaidi, kadri ya tumaini lao kwako na kwa ahadi zako. Mwanao Yesu
Kristu Mwenyewe atawaleta kama utukufu wake, tangu wakati huu wakiwa bado hapa
duniani. Lakini hasa saa yao ya kufa. Amina
x
0 Comments