Maneno
ya Mwokozi wetu: “Leo niletee roho za watu walio wapole na wanyenyekevu wa
moyo, pamoja na roho za watoto wadogo, na uzizamishe katika kilindi cha Huruma
yangu. Roho hizi hufanana kwa ukaribu zaidi na Moyo wangu. Watu hawa ndio
walionitia nguvu wakati wa mateso na uchungu wa mahututi yangu. Niliwaona kama
malaika wa duniani, ambao watakesha daima kuabudu katika altare zangu. Kwa
mafuriko yangu, nitawamwagia neema zangu zote, kwa maana ni roho ile tu iliyo
na unyenyekevu inaweza kupata neema zangu. Ninawapendelea watu walio
wanyenyekevu na kuwaamini sana.”
Tuwaombee
watoto wadogo pamoja na roho zile zenye unyofu kama wao.
Ee Yesu mwenye Huruma sana, Wewe Mwenyewe
ulisema: “Jifunzeni kwangu kwa maana Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa Moyo”,
uwapokee ndani ya Moyo wako uliojaa Huruma, watu wote walio wapole na
wanyenyekevu, pamoja na roho za watoto wadogo. Roho hizi hustaajabisha Mbingu
nzima, maana wanapotokea mbele ya Kiti cha Enzi cha Baba wa mbinguni, huwa kama
shada la maua litoalo harufu tamu ya marhamu safi, na kuifurahisha Mbingu
nzima. Mungu Mwenyewe hufurahia manukato yao safi. Roho hizi zina makao ya
daima ndani ya Moyo wako wenye Huruma ee Yesu. Na daima hukuimbia wimbo wa
Huruma na Upendo wako. Amina.
Baba
yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …
Baba wa
Milele, uzitazame kwa macho ya Huruma, roho za watu wote walio wapole na
wanyenyekevu wa moyo, pamoja na roho za watoto wadogo, walioingizwa katika
makao ambayo ni Moyo wa Yesu Mpenzi, ulio na Huruma nyingi. Roho za watu hawa,
hufanana na Mwanao kwa kwa karibu zaidi. Harufu yao tamu ya fadhila
hukufurahisha sana, nayo hupanda ikianzia hapa duniani mpaka kwenye Kiti chako
Kitukufu. Ee Baba wa Huruma na wema wote, ninakuomba, kwa ule upendo ulio nao
kwa roho hizi penzi, na kwa ajili ya furaha uipatayo kwao, utubariki sisi na
dunia nzima, ili sote pamoja tuungane katika kuisifu Huruma Yako, kwa milele
yote. Amina
0 Comments