Machapisho yanayopendwa

6/recent/ticker-posts

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TATU

 


Maneno ya Bwana Yesu: “Leo niletee roho za watu wenye uaminifu na uchaji wa Mungu, na uwazamishe katika Bahari Kuu ya Huruma yangu. Roho za watu hawa ndizo zilizonifariji katika njia ya Msalaba. Wao ndio waliokuwa tone lile la faraja nilipokuwa katikati ya bahari ya uchungu na mateso.”

Tuwaombee watu wote waaminifu na wenye ibada ambao walimtuliza Yesu katika mateso yake.

Ee Yesu mpole na mwenye huruma sana, Wewe huchota neema kwa wingi kutoka katika hazina Yako, na kuzigawa kwa ukarimu kwa kila mmoja wetu na kwa watu wote. Tunakuomba utupokee katika makao ya Moyo wako mpole na wenye huruma nyingi, na usituache tutoroke humo kamwe. Tunakuomba neema hii, kwa ajili ya mapendo ya ajabu, yawakayo moyoni mwako kwa Baba yako wa mbinguni. Amina

Baba yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …

Baba wa Milele, elekeza macho yako yenye huruma, kwa watu wote walio waaminifu, kama vile kwenye hazina na urithi wa Mwanao. Kwa ajili ya mateso yake ya kuhuzunisha, uwajalie Baraka zako, na ulinzi wako daima. Kwa njia hii, waweze kuimarika katika upendo, na wala wasije wakapoteza hazina bora ya Imani Tashi Takatifu, bali, pamoja na majeshi yote ya malaika na watakatifu, waweze kuisifu na kuitukuza huruma yako isiyo na mwisho, kwa milele yote. Amina

Post a Comment

1 Comments