Maneno
ya Mkombozi: “Leo niletee roho za ndugu waliojitenga na Kanisa, na
uwazamishe katika Bahari Kuu ya Huruma yangu. Wakati ule wa mateso yangu
makali, watu hawa waliurarua mwili wangu na roho yangu, yaani Kanisa langu.
Pindi warudipo tena katika Umoja wa Kanisa, majeraha yangu hupona, na kwa njia
hii wanapunguza ukali wa mateso yangu”.
Tuwaombee
wale waliopotoka katika Imani Katoliki na kujitenga na Kanisa.
Ee Yesu
Mpole na mwenye Huruma, Wewe u Huruma na Wema wenyewe, hukatai kuwapa mwanga
wale wote wanaoutafuta. Uzipokee ndani ya Moyo wako wenye Huruma, roho za ndugu
zetu waliojitenga. Uwavute kwa mwanga wako, ili warudi tena katika Umoja wa
Kanisa lako Takatifu, na uwadumishe humo, wasiweze kutoroka tena Moyo wako
wenye Huruma sana, bali uwawezeshe wao pia pamoja nasi, kuusifu na kuutukuza
ukarimu wa Huruma Yako Kuu, kwa milele na milele. Amina.
Baba
yetu … Salamu Maria … Atukuzwe …
Baba wa
Milele, uzielekee kwa macho ya huruma, roho za ndugu zetu waliojitenga na
Kanisa lako Takatifu, hasa wale waliozitapanya Baraka zako na kuzitumia vibaya
neema zako, kwa kuendelea kishupavu katika mafundisho yao ya upotofu.
Usiyaangalie hayo makosa yao, bali uutazame upendo wa Mwanao Mpenzi, pamoja na
mateso yake makali aliyovumilia kwa ajili yao. Watu hawa pia, wameingizwa ndani
ya Moyo wa Yesu Mwanao, wenye Huruma Kuu. Uwawezeshe vile kwamba, wao pamoja na
sisi sote, tuisifu na kuitukuza Huruma Yako Kuu, kwa milele na milele. Amina
0 Comments