Ibada kwa Bikira Maria Mtakatifu ni moja kati ya njia kuu za wokovu. Mtakatifu Alphonsus Maria Liguori aiiandika katika moja ya vitabu yake: "Mtumishi mcha Mungu wa Maria hataangamia kamwe." Jambo kuu ni kuendelea kuwa waaminifu hadi kifo katika ibada hii kwa Bikira Maria.
Je, ungependa kumwona Mama Bikira kabla
ya kufa? Hapa kuna ibada rahisi ambayo Bikira Maria mwenyewe alimfundisha
Mtakatifu Mechtilde mwaka 1270. Ibada
hii inajulikana kama "Ibada ya Salamu Maria Tatu," na
inajumuisha kusali Salamu Maria tatu kila siku na kisha kusali kwa kusema "Ewe
Mama yangu, unikinge na dhambi ya mauti mchana huu (au usiku)".
katika Ibada hii Salamu Maria inasaliwa mara tatu kwa heshima ya Utatu
Mtakatifu, ambao ndiyo chanzo cha ukuu wote wa Mama Yetu Bikira Maria. Ibada
hii inakusudia kuheshimu Nguvu za Mungu Baba, Hekima ya Mungu Mwana, na Wema wa
Mungu Roho Mtakatifu, kwa ukarimu kwa
Mama Yetu Mbarikiwa.
Ibada hii ilifunuliwa na Mama Yetu Bikira
Maria mwenyewe kwa mtawa Mbenedikto, Mtakatifu Mechtilde. Katika Kitabu cha
Ufunuo wa Mtakatifu Mechtilde tunasoma:
"Wakati Mechtilde
alipokuwa akiomba msaada wa Bikira Mtukufu pale saa yake ya kifo itakapofika,
Mama Yetu alimtokea na kusema: 'Nitakusaidia hakika. Lakini pia nataka usali
Salamu Maria tatu maalumu kwangu kila siku.
'Ya kwanza itakuwa kwa heshima
ya Mungu Baba, Ambaye nguvu zake zote ziliinua Roho yangu juu sana kuliko
kiumbe kingine chochote kwamba, baada ya Mungu, mimi nina nguvu kubwa zaidi
mbinguni na duniani. Katika saa yako ya kifo, nitaitumia nguvu hiyo ya Mungu
Baba kuweka mbali nguvu yoyote ya giza.
'Salamu Maria ya pili itasaliwa
kwa heshima ya Mungu Mwana, Ambaye alinipa hekima Yake isiyoelezeka. Katika saa
yako ya kifo, nitaijaza Roho yako na nuru ya hekima hiyo, ili giza lote la
ujinga na makosa litoweke.
'Salamu Maria ya tatu itakuwa kwa heshima ya Mungu Roho Mtakatifu, Ambaye alijaza Roho yangu na tamu ya upendo Wake na huruma. Katika saa yako ya mwisho, nitabadilisha uchungu wa kifo kuwa tamu ya kimungu na furaha."
Mwandishi wa ufunuo wa Mtakatifu Mechtilde alikuwa ni Mtakatifu
Gertrude Mkuu, Alikuwepo wakati Mtakatifu Mechtilde alipokufa na aliona Bwana
wetu akimtokea. Baadaye, ufunuo mwingi kuhusu Ibada ya Salamu Maria Tatu
ulifunuliwa kwa Mtakatifu Gertrude pia.
Katika Sherehe ya Kupashwa Habari Bikira Maria mnamo 1299, wakati wimbo wa Ave Maria ulipokuwa ukiimbwa Kanisani,
Mtakatifu Gertrude aliona maono ya miale mitatu ya mwanga iliyokuwa ikitoka kwa kila nafsi tatu za Utatu Mtakatifu, miale
hiyo aliiona ikipenyeza Moyo wa Bikira Mtakatifu, kama miale mitatu. Alielewa
kuwa miale mitatu yenye kung'aa ilikuwa alama kwamba: "Baada ya Nguvu
za Baba, Hekima ya Mwana, na Huruma ya Roho Mtakatifu, hakuna kinachokaribia
Nguvu, Hekima, na Huruma ya Maria."
Kisha aliona miale mingine ikirudi kwenye
chanzo chake cha kwanza, na alifunuliwa kujua kwamba hizo zilikuwa neema ambazo
Mama Yetu anawapa wale wanaosali Sala ya
Salamu Maria kwa ibada.
Siku nyingine Bikira Maria alimtokea Mt.
Gertrude na kusema:
"Kwa nafsi yoyote inayosali Salamu
Maria Tatu kwa uaminifu, nitamtokea saa ya kifo katika utukufu wa ajabu sana
kwamba nitajaza Roho ya Mtu huyo na
faraja ya mbinguni."
Mtakatifu maarufu Anthony wa Padua
alikuwa ni Mmoja wa watu wa kwanza kufanya
Ibada hii ya Salamu Maria tatu na kuzipendekeza kwa wengine, Lengo lake maalumu
katika ibada hii lilikuwa kuheshimu Ubikira safi wa Maria na kudumisha usafi
kamili wa akili, moyo, na mwili katikati ya hatari za ulimwengu. Baadae watakatifu
wengi, kama yeye, walifanya ibada hii. Mtakatifu Leonard wa Port Maurice,
mhubiri maarufu (1675-1751), alishauri wasikilizaji wake wote kuzingatia ibada
hii. Alitoa sala hizi za Salamu Maria tatu kama toba katika maungamo, ili kupata neema ya
kuepuka dhambi zote za mauti wakati wa mchana au usiku, hasa kwa wale waliokuwa
wakipambana na dhambi za uchafu; zaidi ya hayo, aliahidi kwa namna maalum,
wokovu wa milele kwa wale wote waliokuwa waaminifu kwa ibada hii.
Baada ya mfano wa watakatifu hao wawili
wa Kifrancisko, Mtakatifu Alphonsus Maria Liguori alikubali ibada hii nzuri na
kuieneza ibadah ii kwa bidii na nguvu. Alishauri matumizi yake, na hata aliwapa
kama toba kwa wadhambi. Ibada hii pia aliizungumzia katika kitabu chake kizuri
na maarufu “The Glories of Mary”.
Mmoja wa waeneza ibada hii maarufu
alikuwa Mkapuchini, Padre John Baptist wa Blois. Na Ilikuwa kwa sababu ya kazi
yake katika kueneza Ibada hii kwamba
Papa Leo XIII alihalalisha ibada hii. Huko Blois alianzisha Kundi linaloitwa "Pia
Opera kwa Uenezi wa Salamu Maria Tatu." Ibada hii Iliidhinishwa na
Maaskofu wengi, kwa muda mfupi ikawa imeenea katika nchi nyingi. Baadaye, mnamo
Julai 30, 1921, Papa Benedict XV, katika barua ya Kitume, aliiinua hadhi ya
Ibada hii akiipatia Rehema nyingi sala
hii.
0 Comments